Sunday, March 30, 2014


Ulevi mbalimbali kwa sasa umeingia vijijini tena unavutwa bila uoga,zamani ulevi vijijini walikuwa wanatumia Pombe,Bangi,Mirungi na nk.
Lakini kwa miaka hii ya sasa kumeingia ulevi mkubwa sana Unga.
Unga sasa umekuwa ulevi mkubwa sana vijijini,vijana wengi wameharibika kwa ulevi huu hatari,
Nguvu kazi imepotea,Uwizi umeongezeka kwa kasi kubwa,vijana wamekuwa vibaka,wezi wa Nazi na vitu vingine.Amani imepotea vijijini,vijana wanarudisha nyuma maendeleo ya jamii kwani wanaiba mali za Umma,Mali za majumbani kwao ilimradi wapate pesa ya kununulia Unga.
Ina wabidi wafanye kazi rahisi ya kuiba kwani afya zao haziruhusu kufanya kazi ngumu.
Wanakijiji wanashindwa kuchukua hatua au maamuzi makali kwa sababu wanajuana au wanaoneana aibu eti kisa ni mtoto wa fulani,Je tutafika

Saturday, March 29, 2014

Manchester United yaichapa Aston villa mabao 4-1.
Leo kulikuwa na mechi kali kati ya Man U na Aston villa mida ya saa 9:30 alasiri,dk ya 10 Aston villa yaanza kupata goal la kwanza.mechi iliendelea kuwa ngumu mno mnamo dk ya 40 Rooney iliipatia Man U bao la 1,ikawa 1-1,Dk ya 45 kwa mara nyingine tena Rooney iliipatia Man U bao la 2,
Baada ya kurud Half time mechi iliendelea kuwa ngumu mno kwa mashuti ya hapa na pale,
Mnamo dk ya 80 Juan Mata aliipatia timu yake bao la 3 na game ilikuwa na mashambulia makali,Aston villa japokuwa ilifungwa bao hayo lakin haikukata tamaa iliendelea kuishambulia Man U.
Lakin Man U haikukubali na kuendeleza ubabe dk ya 90 Chicharito akizidi kuikandamiza Aston villa bao la 4 kuunganissha cross kali iliyopigwa na Junujaz,game iliishia kwa 4-1.

Thursday, March 27, 2014

Serikali yetu imelitilia mkazo suala la elimu na serikali ikaamua kujenga seondary kila kata ktk mikoa yote Nchini tangu mwaka 2004 na kuendeleaserikali ilifanikiwa zoezi hili kwa hali na mali.
Na wanafunzi walifanikiwa kufaulu ktk shule hizo.
Tatizo kubwa lipo ktk kufaulisha form four kwenda form five hapo ndipo kuna mtihan mkubwa mno,
Wananchi wanajiuliza maswali mengi sana kuhusu suala la ufaulu wa watoto wao.
1.Je tatizo ni walimu hawana viwango vya kufundisha? au
2.Walimu ni wachache shuleni? au
3.Tatizo ni vitendea kazi hakuna?au
4.Wanafunzi hawajisomea watokapo shuleni?au
5.Serikali inataka kuunda raia wanaojua kusoma na kuandika tu?
Maswali haya wazazi wanajiuliza kila leo lakin bado hawajapata majibu halisi.
wazazi wanakubali kujinyima mambo mengi lakin mwanae asome na afike mbali ili apate mafanikio matokeo yake mtoto anaishia form two au form four.
Swali langu Je tufanyeje ili kuongeza ufaulu ktk shule zetu za kata?
                                                        MTAZAMO WANGU
Serikali tayari imeshatuonesha njia ya kufuata,tunachotakiwa wananchi tujitolee wenyewe kama tulivyojitolea ktk ujenzi wa majengo ya shule yaani nguvu kazi mtoto asome.
Wananchi tukae tujadili na tuangalie mapungufu yako wapi alafu tuyatatue kidogo kidogo,
Kutokana na mtazamo wangu huyo Inshallah huenda tukapata majibu ya maswali yetu.
Kama una maoni,ushauri tunaomba ucomment ili tupate ufafanuzi....................  


Tuesday, March 25, 2014

Man U vs Man city zakutana tena leo kwa mechi ya marudiano, leo Man United yuko nyumbani Old Trafford akitaka kulipiza kisasi mechi zilizopita je ataweza...??,usikose kufuatilia mchezo huu wa leo utakao chezwa saa 4:45 usiku, pia usikose kutembelea ktk blog hii kupata taarifa mbalimbali. Man U itamkosa mchezaji wake hatari mwenye uchu wa magoli Robin Van Persie aliumia mechi iliyopita Ni majeruhi na yupo nje kwa wiki sita.

Sunday, March 23, 2014

Jana Arsenal yachezea kichapo cha Mbwa mwizi bila huruma tena bila kuangaliwa usoni,imechezea kichapo cha mabao 6-0 ndani ya nyumbani Stamford Bridge.
dakika ya 4 Mu Africa mwenye njaa ya magoli Samuel Etoo afunga bao  la kwanza,mpira ukiendelea kwa kasi mnamo dakika ya 6 Edin Hazard atumbukiza goal la pili kwa mkwaju wa penalt na Gigs akitolewa nje kwa card nyekundu hapo Chelsea ilipamba moto,dakika ya 33 Schurrle akifunga bao la 3 na dakika ya 45 Osca akicheza na nyavu bao la 4.
Kipindi cha pili  dakika ya 65 Osca alicheza na nyavu kwa mara ya pili na mpira ulizidi kuwa mgumu kwa upande wa Arsenal na kuanza kukata tamaa ya kurudisha magoali hayo.
Mnamo dakiaka ya 83 M.Salah akizidi kuwachosha wachezaji wa Arsenal kwa kuongeza bao la 6.
Mchezo uliishia hivyo kwa magoli 6-0,poleni sana washabiki wa Arsenal


Timu hizo jana zilicheza ktk viwanja tofauti tofauti na zilifanikiwa kushinda na kuchukua point 3 muhimu,
(1)Chelsea na Arsenal ziliingia uwanjani mida ya saa 9:30 alasiri,Chelsea ilimchapa Arsenal kipigo cha Mbwana mwizi bao 6-0.
(2)Man United na West hum nazo ziliingia uwanjani mida ya saa 2:30 Man U ikiwa ugenini ilichukua point 3 muhimu kwa kuichapa West hum 2-0.
(3)Liverpool na Cadiff United ziliingia uwanjan mida ya saa 12:30,Liverpool nayo yachukua point 3 kwa kuichapa Cadiff 6-3 mechi hii ilikuwa ngumu mno kwan ilikuwa na ushindan mkubwa sana kila mtu alikuwa akihitaj point 3 muhimu.
(4)Man city na Fulham ziliingia uwanjan mida ya  saa 15:00,Man city ilichukua point 3 kwa kuichapa Fulham mabao 5-0,mechi hii Fulham ilihemewa vibaya mno na kushindwa kupata hata bao kufuta machozi.

Saturday, March 22, 2014

Leo j.mosi ratiba yaendelea tena ktk viwanja mbalimbali
CHELSEA vs ARSENAL
Mida ya saa 9:30 alasiri usikose mechi kali za leo.

LIVERPOOL vs CADIFF
Mida ya saa 12:30 jioni

MAN U vs WEST HAM
Mida ya saa 2:30 usiku
je leo Man U itashinda tena?usikose kufuatilia mchezo huu mkali mno pia usikose kufuatilia blog hii ili kujua matokeo mbali mbali kuhusu michezo hii na habari nyingine tele.
pia michezo mingine kama Man city n.k

Ni Juma Mohammed (J.Tozz),amezaliwa Tanga,wilaya ya Mkinga kijiji cha Magaoni,
Amesoma shule ya msingi Bawa,Kwale sec school,chuo Datastar Training College,
Kwa sasa anaishi Arusha kama Director Ancester Travel and Tours.
Kwa waliopo Arusha kama unamaoni,ushauri na habari yoyote wasiliana nae kwa
 Tell: +255 714 178 093
 Email: kampeni38@gmail.com
 skype: jumamody
 Twiter:jumamody
Pia kama una matangazo mbali mbali usisite kuwasiliana nasi.

Friday, March 21, 2014

Mawasiliano kwa Wadau wa Fikra za Wadigo blog.
 Tell: +255/717 105 505
         +255/783 105 505
          +255/716 568 163
Email:  Kidemanho@gmail.com
           Mwadambo@gmail.com
           fikrazawadigo@wadigo.com
Website: w.w.w.fikrazawadigo.co.tz
Kama una maoni,habari,ushauri au kama unataka kujiunga ili uwe unaandika habari mbali mbali wasiliana nasi.
Nawatakia Ijumaa njema Waislam wote dunia,Mungu azikubali swala na dua zenu,
Pia nawahasi tufike misikitini mapema ili kupata fadhila za Ijumaa,
tufunge biashara zetu kwa muda pia tuwah hotuba 2 muhimu kabla ya swala,Mtume Muhammad (s.aw)
anatuhimiza pindi tuendapo Ijumaa basi tuoge,kwahiyo tusisahu kuoga kwa siku ya leo pia tujipake manukato kama tunayo,tukumbuke kuvaa nguo nzuri hasa hasa Kanzu kwa wanaume.
                                                       IJUMAA KAREEM.

Mwandishi wetu na mtoaji habari mbalimbali ktk Blog yetu ya Wadigo kule visiwani Pemba ni MUSSA MWADAMBO, Huyu ni kijana mdogo sana aliyezaliwa Mkoa wa Tanga wilaya ya mkinga kata ya kwale kijiji cha Kichalikani, pia amesoma shule ya msingi Vyeru na akafaulu shule ya secondary Kwale. Kwa sasa anaishi Pemba pamoja na shughuli zake zote anafanyia kule. Kwa walio visiwani kama una habari,Maoni,ushauri kuhusu blog yetu Muone Mr.Mussa Mwadambo au wasiliananae kwa Tell: +255/716 568 163 +255/776 347 877 Email:Mwadambo@gmail.com Kijana huyu ni rafiki mkubwa wa Kidema au Kidemanho ambae pia ni Muandishi wetu aliyepo Daressalam, Ni marafiki tokeo wanasoma Nursery,Primary na Secondary

Thursday, March 20, 2014

Shule ya secondary Kwale iliyopo mkoa wa Tanga wilaya ya Mkinga kata ya Kwale iliyoanzishwa mwaka 2005,2006 matokeo yake ya mwaka 2013 yamekuwa yakitishia amani, ziro ni nyingi mno kuliko walio pata alama ya kupata cheti cha kumaliza elimu ya kudato cha nne,Wazazi wengi wakilalamika na kukata tamaa juu ya kizazi kijacho. Shule hii ilikuwa na matokeo mazuri sana hapo awali ilifaulisha vijana mwaka 2009,2010 na 2011 wengine wapo mavyuoni,Makazini nk. MAOMBI YA WANANCHI Wanaomba wadau wenye uchungu na maendeleo ya kata yao wafanye mpango wa kuongeza walimu, pamoja na vifaa vya utendaji kazi kama vitabu,chalks,madawati na maabara. Pia wanafunzi waliopo mavyuoni na wale wa form 5 na 6 wajitolee kuja kufundisha ndugu zao

Wednesday, March 19, 2014

Manchester United yafuzu kuingia robo fainal baada ya kuichapa Olympiokos magoli 3-0. Magoli hayo yakifungwa na V.Persie ktk dk ya 25 kwa mkwaju wa Penalt na dk ya 45 ktk kipindi cha kwanza.Baada ya kurudi kipindi cha pili dk ya 52 V.Persie aliifungia tena timu yake kwa mkwaju wa faulu ulioingia moja kwa moja wavuni. kwa magoli hayo matatu imeiwezesha Man U kuingia Robo fainal
Shule ya secondary Kwale iliyopo mkoa wa Tanga wilaya ya Mkinga kata ya Kwale iliyoanzishwa mwaka 2005,2006 matokeo yake ya mwaka 2013 yamekuwa yakitishia amani, ziro ni nyingi mno kuliko walio pata alama ya kupata cheti cha kumaliza elimu ya kudato cha nne,Wazazi wengi wakilalamika na kukata tamaa juu ya kizazi kijacho. Shule hii ilikuwa na matokeo mazuri sana hapo awali ilifaulisha vijana mwaka 2009,2010 na 2011 wengine wapo mavyuoni,Makazini nk. MAOMBI YA WANANCHI Wanaomba wadau wenye uchungu na maendeleo ya kata yao wafanye mpango wa kuongeza walimu, pamoja na vifaa vya utendaji kazi kama vitabu,chalks,madawati na maabara. Pia wanafunzi waliopo mavyuoni na wale wa form 5 na 6 wajitolee kuja kufundisha ndugu zao
Vijana wa kidigo wa kijiji cha Kichalikani wakipeana mawazo mbali mbali ya kuhusu maisha ya mjini,vijana hawa wanashirikiana kwa kila jambo na wanapanga mikakati madhubuti kuhusu maendeleo ya kijiji chao kichalikani. kijiji chao kwa sasa kina mafanikio makubwa,vijana wameilimika wamejenga ya msingi, wanajenga nyumba madhubuti za tofali na sasa wanampango wa kujenga Hospital ya kijiji.
Real Mardid yafuzu ktk mchezo wa jana kti ya Shalk o4 kwa kuichapa mabao 3-1. Mchezo ulikuwa mgumu sana hadi half time bao ni 1-1,baada ya kurud tena dumbani Mchezajio bora wa dunia C.Ronald akaipatia timu yake bao la pili mnapo dk ya 67, mchezo uliendelea kuw mgumu sana. kwenye dk ya 83 mchezaji ISCO akaipatia tena yake bao la 3, mpaka kipenga cha mwisho Real Madrid waliondoka na ubingwa huo.

Monday, March 3, 2014

Wavuvi wa kijiji cha kichalikani wakitoka Bahari, wakishirikiana ili kuleta maendeleo yao kijiji chao, tayar wameshaanza kujenga shule yao ya msingi, sasa wana hamu ya kujenga Hospitali yao ya kijiji. Karibuni sana Kichalikani.